UZINDUZI WA MAGARI MAPYA YA KAMPUNI YA ULINZI YA SUMAJKT GUARD LIMITED

...
...
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi Kujenga Taifa SUMAJKT Brigedia Jenerali Petro Ngata, Kwa niaba ya Afisa Mtendaji Mkuu wa SUMAJKT Meja Jenerali Rajabu Mabele, amezindua magari idadi Ishirini na mbili ya Kampuni ya Ulinzi SUMAJKT Guard Limited. Uzinduzi huo umefanyika Februari 13, 2026 Makao Makuu ya Shirika Mlalakuwa Dar es salaam, ambapo Brigedia Jenerali Petro Ngata, ameeleza ushirikiano uliopo kati ya SUMAJKT na wadau mbalimbali wa kibiashara ndio msingi wa mafanikio ya Shirika.